Mazingira FM

Wananchi watakiwa kutosusia mikutano ya kampeni

24 September 2025, 5:32 pm

Dkt Thomas Masanja Kamishna wa Tume ya haki za binadamu na Utawara Bora

Wananchi watakiwa kujitokeza kwenye mikutano ya kampeni ya wagombea ili kusikiliza sera zao

Na Adelinu Banenwa

Wito umetolewa kwa wananchi kujitokeza kwenye mikutano ya kampeni ya wagombea ili kusikiliza sera zao zitakazowawezesha kuchagua viongozi bora.

Hayo yamesemwa leo tarehe 24 September 2025 na Dkt Thomas Masanja ambaye ni Kamishna wa Tume ya haki za binadamu na Utawara Bora katika kipindi cha Asubuhi leo Kinachorushwa hapa radio mazingira fm

Sauti ya Dkt Thomas Masanja Kamishna wa Tume ya haki za binadamu na Utawara Bora
Majid Kangile, Afisa sheria wa  Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

Kwa upande wake Majid Kangile ambaye ni afisa sheria wa  Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora amesema zipo faida mbalimbali za wananchi kushiriki uchaguzi pia kuudhuria kampeni za wagombea

pia Majid amesema zipo hasara kwa wananchi kutokuudhuria kampeni za wagombea pia kutokupiga kura hivyo ametoa rai kwa wananchi wote kuhakikisa wanashiriki katika uchaguzi huu ili waweze kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo.

Sauti ya Majid Kangile, Afisa sheria wa  Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
Joel John, Mkurugenzi mkuu wa ndani Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

Naye Joel John Mkurugenzi mkuu wa ndani Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora amesema kwa mujibu wa utaratibu mwannachi anazo haki mbalimbali katika kipindi hiki cha uchaguzi ikiwemo haki ya kujiandikisha.

Sauti ya Joel John Mkurugenzi mkuu wa ndani Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora