Mazingira FM

Visa magonjwa ya kuhara, kutapika vyaripotiwa kwa wingi Bunda

18 September 2025, 1:12 pm

Magreth Nyambwa afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Bunda na Afisa afya wa halmashauri ya mji wa Bunda Wilfred Gunje wakiwa studio radio Mazingira fm,picha na Catherine Msafiri

Afisa afya halmashauri ya mji wa Bunda Wilfred Gunje amebainisha kuwa magonjwa ya mlipuko ni magonjwa yanayotokea kwa ghafla na kuenea kwa haraka kama,covid 19 ,homa ya manjano,ebola na kuhara na kutapika

Na Catherine Msafiri

Serikali imeweka mikakati katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kwa kutoa elimu kwa jamii namna ya kukabiliana,kuandaa kambi ya madaktari ili kusaidia kutoa msaada kwa wagonjwa wanaobainika na dalili ama magonjwa ya mlipuko.

Hayo yameelezwa na Magreth Nyambwa afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara wakati akizungumza kwenye kipindi cha kapu letu kinacholuka radio mazingira fm kuhusu namna ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ambapo ameeleza kuwa serikali imejipanga katika kuhakikisha inakabiliana na magonjwa hayo.

Sauti ya Magreth Nyambwa afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Bunda

Awali afisa afya wa halmashauri ya mji wa Bunda Wilfred Gunje akieleza magonjwa ya mlipuko amebainisha kuwa magonjwa ya mlipuko ni magonjwa yanayotokea kwa ghafla na kuenea kwa haraka kama,covid 19 ,homa ya manjano,ebola na kuhara na kutapika.

Sauti ya Afisa afya wa halmashauri ya mji wa Bunda Wilfred Gunje

Aidha maafisa afya hao wamebainisha kuwa katika halmashauri zote mbili za wilaya ya bunda wamekuwa wakipokea kwa wingi wagonjwa wa kuhara na kutapika.

Sauti za Afisa afya wa halmashauri ya wilaya na mji wa Bunda

Hata hivyo wamebainisha kuwa serikali inashiriki kikamilifu katika Siku ya Usafishaji Duniani (World Cleanup Day) ambayo huadhimishwa jumamosi ya tatu ya mwezi Septemba kila mwaka,ikiwa na lenga kuhamasisha jamii duniani kote kushiriki katika kampeni za usafi wa mazingira, kupunguza taka na kulinda mazingira.

Huku maadhimisho ya mwaka huu yakiwa na kauli mbiu isemayo “Tunza mazingira ,kwa kuzipa taka thamani” .