Mazingira FM

Ni marufuku taasisi binafsi kuuza magari yenye msamaha wa kodi

12 September 2025, 11:47 am

Geofrey Commoro afisa elimu kwa mlipa kodi na mawasiliano wilaya ya Bunda,picha na Joseph Makori

Kwa mujibu wa kifungu cha 70(1) cha sheria ya utawala wa kodi sura 438 na kifungu cha 249 cha sheria ya forodha ya jumuiya ya Afrika mashariki ya mwaka 2004 ,

Na Catherine Msafiri,

Imeelezwa kuwa mamlaka ya mapato Tanzania TRA imekuwa ikikabiliana na changamoto za usimamizi wa magari yasiyokidhi matakwa ya sheria ya dirisha ambayo hayalipiwi ushuru na kodi husika wakati wa kuingizwa nchini

Kwa mujibu wa kifungu cha 70(1) cha sheria ya utawala wa kodi sura 438 na kifungu cha 249 cha sheria ya forodha ya jumuiya ya Afrika mashariki ya mwaka 2004 , kamishna mkuu wa Mamlaka ametoa msamaha wa kodi kwa wamiliki wa magari ambayo yakiingizwa nchini kwa kujua au kutokujua kwamba haya kulipiwa ushuru na kodi kikamilifu

Afisa wa forodha mkoa wa Mara Iddi Gubwe na Geofrey Commoro afisa elimu kwa mlipa kodi na mawasiliano ,picha na Joseph Makori

Akizungumza kuhusu msamaha huo kwenye kipindi cha kapu letu kinacholuka radio Mazingira fm,afisa wa forodha mkoa wa Mara Iddi Gubwe amewataka wamiliki wa magari ya taasisi binafsi kuacha tabia ya kuuza magari yenye msamaha wa ushuru wa forodha bila kufuata masharti

sauti ya Iddi Gubwe Afisa wa forodha mkoa wa Mara Iddi Gubwe

Kwa upande wake Geofrey Commoro afisa elimu kwa mlipa kodi na mawasiliano wilaya ya Bunda amewaasa walipa kodi wote kuomba msamaha ndani ya miezi hiyo iliyoweka

sauti ya Geofrey Commoro afisa elimu kwa mlipa kodi na mawasiliano

Hata hivyo TRA imetoa msamaha wa kodi kwa kipindi cha kuanzia tarehe 01 Augost 2025 hadi 31Disemba,2025 , miongoni mwa magari hayo ni magari yaliyoingizwa mchini kwa muda na hayakuweza kurudishwa yalikotokea, magari yaliyoingia Tanzania bara kutokea Zanzibar bila kufuata taratibu za kiforodha na magari yaliyosamehewa kodi lakini umiliki wake umehamishwa kwenda kwa mmiliki mwingine .