Mazingira FM
Mazingira FM
11 September 2025, 9:04 pm

“Inaonesha mzee huyo amejinyonga kutokana na msongo wa mawazo kwa kuwa ni kama familia yake ilikuwa haimjali”
Na Adelinus Banenwa
Mzee mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Odondo mwenye umri wa miaka 93 mkazi wa kijiji cha Nyaburundu kata ya Ketare halmashauri ya wilaya ya Bunda amekutwa amefariki kwa kujinyonga chumbani kwake kisa kikidaiwa kuwa ni msongo wa mawazo na kutelekezwa na familia.
Akizungumza na redio Mazingira FM mwenyekiti wa kijiji hicho ndugu Hamis Saidi Madoro amesema ni kweli tukio hilo limetokea na taarifa za tukio hilo amezipata leo asubuhi akiwa shambani baada ya kupigiwa simu na mwenyekiti wa kitongoji na alipofika eneo la tukio ni kweli alikuta mzee huyo amening’inia.
Madoro amesema inaonesha mzee huyo amejinyonga kutokana na msongo wa mawazo kwa kuwa ni kama familia yake ilikuwa haimjali licha ya kuwa alikuwa kwenye mpango wa kuzinusuru kaya masikini yaani TASAF lakini bado alikuwa anaishi katika mazingira magumu.
Aidha mwenyekiti huyo ametoa rai kwa wananchi kujenga tabia ya kuwatunza wazee na kuwasaidia ili kuepusha watu hao kuchukua maamuzi magumu kutokana ana msongo wa mawazo na kukosa huduma.