Mazingira FM
Mazingira FM
9 September 2025, 8:38 pm

Aretas amesema mtuhumiwa huyo alikuwa akitafutwa kutokana na matendo yake ya kuendelea kuzalisha na kuuza bangi kinyume na sheria.
Na Adelinus Banenwa
Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini imemkamata Masero Ryoba Muhabe 44 anayetajwa kuwa kinara wa uzalishaji na uuzaji wa dawa za kulevya aina ya bangi mkoani Mara na nchi jirani.
Aretas Lyimo Kamishan Jenerali wa mamlaka ya kudhibiti na kupambana na na dawa za kulevya amesema Muhabe mkazi Tarime mkoani Mara alikamatwa na mamlaka hiyo akiwa na tani 6.5 za bangi ambazo zilikuwa tayari kwa kusafirishwa.
Aretas amesema mtuhumiwa huyo alikuwa akitafutwa kutokana na matendo yake ya kuendelea kuzalisha na kuuza bangi kinyume na sheria pia amekuwa akishawishi watu wengine kuendelea na biashara hiyo akidai hakuna watakachofanywa.
Kamishna Lyimo amesema katika tukio jingine mkoani Mara mamlaka hiyo imemkamata Simon Gerevas mkonda 51 akiwa na kilo 193 za bangi pamoja na silaha aina ya bastora ikiwa na risasi 11 ambayo alikuwa akiimiliki kinyume nasheria kwa lengo la kulinda biashara zake hizo haramu za usafirishaji wa dawa za kulevya.