Mazingira FM

Udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano ni shida

5 September 2025, 6:09 am

Afisa lishe wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Martin Elias

Sababu kuu zinazopelekea udumavu kuwa ni pamoja na lishe duni hasa katika kipindi cha za mwanzo tangu mama anapopata ujauzito  hadi mtoto anapotimiza umri wa miaka miwili, 

Na Therezia Thomas

Afisa lishe wa Halmashauri ya Mji wa Bunda kwa niaba ya Afisa Lishe wa Mkoa wa Mara Martin Elias ameeleza kuwa hali ya udumavu kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano bado ni changamoto kubwa katika baadhi ya wilaya za mkoa wa Mara, licha ya jitihada mbalimbali za serikali na wadau wa maendeleo.

Akizungumza katika kipindi cha kapu letu kinachorushwa na Mazingira fm mjini Bunda afisa huyo amesema kuwa kwa sasa kiwango cha udumavu katika mkoa wa Mara kimefikia asilimia 23.2

Sauti ya Afisa lishe wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Martin Elias

Amesema moja ya changamoto kubwa inayokwamisha juhudi za kupambana na udumavu ni tabia ya baadhi ya wazazi kutoroka na watoto wao mara tu baada ya kugundulika kuwa wana hali ya utapiamlo au udumavu, hivyo kuwafanya watoto hao wakose ufuatiliaji na huduma muhimu za matibabu na lishe.

Sauti ya Afisa lishe wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Martin Elias

Ametaja sababu kuu zinazopelekea udumavu kuwa ni pamoja na lishe duni hasa katika kipindi cha za mwanzo tangu mama anapo pata ujauzito  hadi anapotimiza umri wa miaka miwili,  umaskini, huduma duni za afya, na uelewa mdogo wa wazazi kuhusu lishe bora.

Afisa Lishe huyo ametoa wito kwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kushirikiana kikamilifu katika mapambano dhidi ya udumavu kwa watoto, akisisitiza kuwa jukumu hilo si la serikali pekee na  kwamba  malezi bora, lishe sahihi, na ufuatiliaji wa huduma za afya kwa watoto vinapaswa kupewa kipaumbele ndani ya familia huku akiwsihi wazazi kuacha tabia ya kutoroka na watoto wakati wa matibabu, kwani hatua hiyo huhatarisha afya na maisha ya watoto.