Mazingira FM

Maboto awaburuza Esther Bulaya na Kambarage kura za maoni

5 August 2025, 6:19 am

Robert Chacha Maboto

Mkurugenzi wa uchaguzi CCM Wilaya ya Bunda Michael Chonya amesema kuwa Maboto amepata jumla ya kura 2,545,

Na Edward Lucas

Ni mbunge anayetetea nafasi yake Robert Maboto amewashinda Esther Bulaya na Kambarage Wasira kura za maoni Bunda Mjini

Robert Chacha Maboto ameibuka mshindi wa kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Bunda Mjini, baada ya kuwashinda wapinzani wake wakuu Kambarage Wasira na Ester Amos Bulaya.

Akitangaza matokeo hayo usiku wa Agost 4, 2025, Mkurugenzi wa uchaguzi CCM Wilaya ya Bunda Michael Chonya amesema kuwa Maboto amepata jumla ya kura 2,545, akifuatiwa na Kambarage Wasira aliyepata kura 2,032, huku Ester Bulaya akishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 625.

Sauti ya Mkurugenzi wa uchaguzi CCM Wilaya ya Bunda Michael Chonya

Wagombea wengine waliokuwa wakichuana katika kinyang’anyiro hicho ni Exavery Lugina aliyepata kura 222 na Joseph Buluba aliyepata kura 159.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi wa kura hizo za maoni Maboto amesema

Sauti ya Robert Chacha Maboto