Mazingira FM
Mazingira FM
4 August 2025, 6:22 pm

kiapo walichokiapa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi mbele ya Mhe hakimu wa mahakama ya Mwanzo Oscar Lyimo ni kujiondoa kuwa mfuasi wa chama chochote cha siasa na pili ni kiapo cha kutunza siri
Na Adelinus Banenwa
Jumla ya wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi 38 halmashauri ya wilaya ya Bunda wamekula kiapo katika semina ya siku tatu yenye lengo la kutoa maelekezo ya namna ya kusimamia uchaguzi mkuu wa 2025.

Wasimamizi hao wasaidizi ngazi ya kata ambao 14 kutoka jimbo la Bunda na 24 kutoka jimbo la Mwibara wanaendelea na mafunzo kwa siku tatu ambayo yameanza leo Augost 4 na yanatarajiwa kumalizika tarehe 6 Augost 2025.

Oscar Mchemwa Msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya wilaya ya Bunda yenye majimbo ya Mwibara na Bunda amesema kiapo walichokiapa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi mbele ya Mhe hakimu Mfawidhi wa mahakama ya Mwanzo Oscar Lyimo ni kujiondoa kuwa mfuasi wa chama chochote cha siasa na pili ni kiapo cha kutunza siri
Naye msimamizi msaidizi wa uchaguzi wa jimbo la Mwibara Rachel Joseph Lazaro amesema wanaamini mafunzo wanayoendelea kuyatoa yanakwenda kuwajengea uwezo kuhakikisha wanatimiza majukumu yao kwa Mujibu wa sheria, kanuni na miongozo ya tume huru ya taifa ya Uchaguzi INEC

Kwa upande wao baadhi ya wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata wamesema wanatarajia mafunzo haya yatawasaidia sana katika kutekeleza majikumu yao pia wanahaidi kutenda haki wakati wote wa kutekeleza majuku yao