Mazingira FM

Msimalize kesi za ukatili kienyeji

26 July 2025, 8:22 pm

Emmanuel Alphonce mkurugenzi wa msaada wa kisheria Musoma

Jamii inatakiwa kubadilika na kuacha kumaliza kesi zaukatili majumbani na kuwaacha wahanga wakibaki na maumivu

Na Adelinus Banenwa

Jamii yashauriwa kuwa na mwamko wa kuripoti matukio ya ukatili wa kijinsia kwenye mamlaka zinazohusika na kuacha kumaliza kesi hizo kienyeji ili kupunguza matukio ya ukatili kwenye jamii.

Hayo yamesemwa leo tarehe 26 july 2025  na wasaidizi wa masuala ya kisheria kutoka musoma wakati wakizungumza kupitia kipindi cha ufahamu wa sheria kinachorushwa na radio mazingira fm.

Emmanuel Alphonce mkurugenzi wa msaada wa kisheria Musoma amesema jamii imekuwa na kasumba kwamba kutoa ripoti za ukatili kunahitaji gharama kubwa jambo ambalo si kweli kwa kuwa wao kama watoa msaada wa kisheria huduma hizo ni bure.

Sauti ya Emmanuel Alphonce mkurugenzi wa msaada wa kisheria Musoma
Debora Sandhu msaidizi wa sheria kutoka Manispaa ya Musoma

Naye Debora Sandhu msaidizi wa sheria kutoka Manispaa ya Musoma amesema jamii inatakiwa kubadilika na kuacha kumaliza kesi zaukatili majumbani na kuwaacha wahanga wakibaki na maumivu badala yake watu watoe taarifa kwenye vyombo husika ili hatua zichukuliwe.

Sauti ya Debora Sandhu msaidizi wa sheria kutoka Manispaa ya Musoma