Mazingira FM
Mazingira FM
16 July 2025, 11:26 am

Vipo vyanzo vya aina tatu vya ajali ambavyo ni Vyanzo vya kibinadamu, Vyanzo vya kimazingira na vyanzo vya kiufundi.
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa kwa watumiaji wote wa barabara wilayani Bunda kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zisizo za lazima.
Hayo yamesemwa na ASP Faustin .J. Buhembere ambaye ni Mkuu wa Usalama barabarani wilaya ya Bunda wakati akizungumza na wananchi kupitia Radio Mazingira FM kwenye kipindi cha Asubuhi leo ambapo amesema ninwajibu wa watumiaji wote wa barabara kuhakikisha wanazingatia sheria za usalama barabarani.

ASP Buhembere amesema vipo vyanzo vya aina tatu vya ajali ambavyo ni Vyanzo vya kibinadamu, Vyanzo vya kimazingira na vyanzo vya kiufundi.
Naye mkaguzi msaidizi wa polisi Emmanuel Joseph ambaye pia ni mkuu wa usalama barabarani msaidizi amesema kama jeshi la polisi usalama barabarani wanalo jukumu la kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya watumiaji wa barabara kupitia njia za mikutano, mashuleni, vyombo vya habari miongoni mwa njia zingine.

Emmanuel amesema kundi ambalo bado linaonekana linahitaji elimu zaidi ni madereva wa pikipiki maarufu bodaboda ambalo limeonekana ni changamoto kwenye kufuata sheria za usalama barabarani.