Mazingira FM

Mbio za mwenge kuwa fursa kwa vijana Bunda

9 July 2025, 5:21 pm

Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda, Salumu Mtelela

Nafasi za ushiriki katika mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2025, ambapo jumla ya vijana saba wanahitajika kushiriki kutoka Wilaya ya Bunda na Mkoa wa Mara.

Na Adelinus Banenwa

Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda, Salumu Mtelela, ametangaza nafasi za ushiriki katika mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2025, ambapo jumla ya vijana saba wanahitajika kushiriki kutoka Wilaya ya Bunda na Mkoa wa Mara.

Kwa mujibu wa Mtelela, nafasi sita zimetengwa kwa vijana wa Wilaya ya Bunda, huku nafasi moja ya kipekee ikiwa kwa msichana mmoja kutoka bunda atakayekimbiza mwenge kimkoa.

Hata hivyo, msichana huyo anatakiwa awe amewahi kushiriki mbio za Mwenge wa Uhuru katika ngazi ya wilaya hapo awali.

Sauti ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda, Salumu Mtelela

Vigezo vya msingi kwa waombaji ni kuwa raia wa Tanzania, wenye umri kati ya miaka 18 hadi 35, wawe wamehitimu elimu ya angalau kidato cha nne, na lazima wawe Skauti, au wawe wamepitia mafunzo ya Mgambo au JKT.

Mchakato wa kupokea maombi utaanza rasmi tarehe 10 Julai na kufungwa tarehe 15 Julai 2025.

Sauti ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda, Salumu Mtelela