Mazingira FM
Mazingira FM
6 May 2025, 3:31 pm

Wananchi ambao vitambulisho vyao vya zamani bado wanavyo na havina shida yoyote ya kufutika au kukatika na hawajahama kata au jimbo hawana haja ya kwenda kutafuta vitambulisho vingine.
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa kwa wananchi wa jimbo la bunda mjini ambao bado hawajaenda kuboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu la mpiga kura katika muda huu uliosalia.
Akizungumza na Mazingira fm afisa mwandikishaji jimbo la Bunda mjini Bi Adelina Mfikwa amesema zoezi hilo linachukua siku saba ambapo lilianza tangu tarehe 1 May na linatarajiwa kuhitimishwa May 7 hivyo kila mwananchi ambaye alikuwa hajajiandikisha au kuboresha taarifa zake kama amehama kata au jimbo au ana ndugu amepoteza maisha ni vema akafika kwenye kituo cha uandikishaji kuboresha taarifa hizo.
Adelina amewatoa hofu wananchi ambao vitambulisho vyao vya zamani bado wanavyo na havina shida yoyote ya kufutika au kukatika na hawajahama kata au jimbo hawana haja ya kwenda kutafuta vitambulisho vingine kwa kuwa hivyo walivyonavyo ni halali


Aidha amewataka wale wote ambao hawajaenda kwenye vituo walivyojiandikisha kwa mara ya kwanza kufanya hivyo ili kuwa na uhakika wa kuwepo kwa majina yao kwenye daftari la kudumu la mpiga kura kwa kuwa ni wale tu walioko kwenye daftari hilo watakuwa na haki ya kupiga kura siku ikifika.