

30 March 2025, 12:58 pm
Kwa mujibu wa kifungu cha 51 na 52 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa sura ya 329 kinaeleza vizuri kwa namnagani taarifa zinazotolewa zinakuwa za siri na maafisa wa takukuru wanazilinda na kumlinda mtoa taarifa.
Na Adelinu Banenwa
Wito umetolewa kwa wananchi kutojihusisha kwa namna yoyote na masuala ya rushwa kuelekea uchaguzi mkuu hali itakayopelekea kupata viongozi bora.
Hayo yamesemwa na Winfrida Kanyika afisa TAKUKURU mkoa wa Mara alipokuwa akizungumza na jamii kupitia kipindi cha ufahamu wa sheria kinachorushwa hapa redio Mazingira Fm.
Winifrida amesema kura ya mwananchi inaweza kuwa sumu ama mbolea ya maendeleo yake na hii inategemea alivyojiandaa kabla ya uchaguzi huo endapo atakubali kumchagua kiongozi kutokana na rushwa basi ni vigumu kupata maendeleo.
Mbali na hayo pia ameitaka jamii kutoa taarifa za rushwa kwenye mamlaka ili wahusika waweze kuchukuliwa hatu ambapo kwa mujibu wa sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa sura 329 kifungu cha 39 cha sheria hiyo inatoa wajibu kwa kila mwananchi kushiriki katika mapambano dhidi ya rushwa hivyo jukumu la kupambana na rushwa si la TAKUKURU pekee.
Akizungumzia ulinzi wa mtoa taarifa za matukio ya rushwa Winfrida amesema kwa mujibu wa kifungu cha 51 na 52 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa sura ya 329 kinaeleza vizuri kwa namna gani taarifa zinazotolewa zinakuwa za siri na maafisa wa TAKUKURU wanazilinda na kumlinda mtoa taarifa.