Mazingira FM

Milioni 187.4 zatolewa kwa vikundi 34 Bunda DC

31 December 2024, 7:18 pm

Viongozi wa wilaya ya Bunda kwenye picha ya pamoja na vikundi vilivyopokea mkopo wa halmashauri wa asilimia 10 kutoka mapato ya ndani halamshauri ya wilaya ya Bunda

Kulipa mikopo kwa wakati na kubaki na mipango iliyopelekea kuomba mkopo kitasaidia vikundi vilivyokopa kupata manufaa na fedha za halmashauri.

Na Adelinus Banenwa

Kiasi cha shilingi milioni 187.4 zimetolewa na halmashauri ya wilaya ya Bunda kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ikiwa ni asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri hiyo.

Shughuli hii imefanyika leo 31 DEC 2024 katika ukumbi wa Halmashauri ambapo zaidi ya vikundi 34 vimenufaika ambapo kati yao 19 vijana,14 wanawake na 1 wenye ulemavu.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mikopo hiyo kaimu mkuu wa wilaya ya Bunda na mkuu wa wilaya ya Tarime Meja Edward Gowele amevitaka vikundi vilivyonufaika na mkopo wa asilimia 10 kuhakikisha wanaendeleza ile mipango iliyopelekea kuomba mkopo badala ya kubadili miradi na mwisho wa siku kushindwa kulipa

Aidha Gowele ameongeza kuwa jambo lingine ni kulipa mikopo hiyo kwa wakati ili kutoa nafasi kwa vikundi vingine pia Sambamba na wao kupata kiwango cha juu zaidi ya kile cha awali.

Sauti ya kaimu mkuu wa wilaya ya Bunda na mkuu wa wilaya ya Tarime Meja Edward Gowele
Vikundi vilivyopokea mkopo wa halmashauri wa asilimia 10 kutoka mapato ya ndani halamshauri ya wilaya ya Bunda

Kwa upande wao baadhi wanachama wa vikundi vilivyobahatika kupata mkopo huo wa asilimia 10 kutoka halmashauri wamesema mikopo hiyo itawasaidia kuepukana na changamoto walizokuwa wakizipata kwenye mikopo umiza ikiwemo ile ya kausha damu.

Aidha wanufaika hao wameishukuru halmashauri ya wilaya ya Bunda pamoja na Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuruhusu utoaji wa mikopo hiyo ya asilimia 10 kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Sauti za baadhi wanachama wa vikundi vilivyobahatika kupata mkopo