TRA yatoa zawadi kwa walipakodi kwa hiari Bunda
20 December 2024, 1:39 pm
Miongo mwa Kampuni zilizopokea zawadi hizo za pongezi ni Kampuni ya Maboto microfanence.
Na Adelinus Banenwa
TRA yakabidhi zawadi za pongezi kwa wateja wake wanaolipa kodi kwa hiari mjini Bunda
Alferd Mregi, Kamishina wa kodi za ndani TRA amewataka wale wenye malimbikizo ya kodi kutimiza wajibu wao kwa kutembelea ofisi za TRA kote nchini, ili kujadiliana na kuingia makubaliano ya ulipaji wa kodi, bila kuathiri shughuli zao za kiuchumi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi za pongezi hizo meneja wa TRA mkoa wa Mara Nasoro Ndemo amesema wao kama mamlaka wanatambua mchango wa wafanyabiashara wanaolipa kodi kwa hiari ambapo miongoni mwao ni Kampuni ya Maboto.
Vestina Benard meneja wa taasisi za Robert Maboto amesema wao kama taasisi wanaishukuru Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan paomoja na TRA kwa kuwapa uhuru na ushirikiano taasisi hiyo hasa katika kuwapa miongozo mbalimbali ya ulipaji wa kodi hali inayowafanya kujituma kulipa kwa wakati .
Aidha vestina amesema kampuni za Maboto zinalipa zaidi ya shilingi bilion 2 kwa mwaka TRA makao makuu hivyo waishukuru TRA kwa kutambua mchango wao .
Katika hatua nyingine, Mregi amewakumbusha wafanyabiashara kutoa risiti za kielektroniki kila wanapouza bidhaa au huduma mbalimbali.
Vilevile, amekumbusha wanunuzi kudai risiti za kielektroniki kwa kila manunuzi ya bidhaa au huduma.