Wezi waiba kwenye maduka zaidi ya 11 Bunda
18 December 2024, 12:24 pm
“Wametoboa signboard wamekunywa soda maganda wametupa hapo chini walinzi walikuwa nje hawakujua kilichokuwa kikiendelea“.
Na Adelinus Banenwa
Ni katika hali isiyo ya kawaida wezi waiba zaidi ya maduka 11 eneo la Genge la jioni mtaa wa Posta kata ya Bunda mjini bila kubomoa wala kuvunja kufuli
Wakizungumza na Mazingira fm baadhi ya wafanyabiashara na wamiliki wa maduka hayo wamesema hali hiyo imegundulika Asubuhi baada ya moja ya wafanyabiashara kugundua kuwa signboard ya duka lake imetobolewa na baadhi ya bidhaa zimeibiwa.
Aidha wafanyabiashara hao wamesema hii si Mara ya kwanza tukio hili kutokea ambapo kwa kumbukumbu katika eneo hilo mwezi February wizi pia ulifanyika eneo hilo na hakuna hatua zilizochukuliwa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Posta kata ya Bunda Mjini Bi Amina Selemani amesema taarifa za tukio hilo amezipata majira ya asubuhi na alipofika eneo la tukio ni kweli aliona uhalifu huo uliotendeka.
Aidha mwenyekiti huyo amesema alilifahamisha jeshi la polisi ambao walifika mapema na wanaendelea na uchunguzi, huku mwenyekiti akitaja kulaani kitendo hicho na kuwatoa hofu wananchi wa Bunda mjini juu ya usalama kuelekea sikukuu za kufunga mwaka 2024