Yas imebadili chapa huduma bado ni zilezile
11 December 2024, 4:32 pm
YAS inaendelea kutoa ofa mbalimbali kuelekea msimu huu wa kufunga mwaka ambapo zipo zawadi ambazo zinatolewa kwa washindi wa kila siku, wiki, mpaka mwezi.
Na Adelinus Banenwa
Wateja wa mtandao wa mawasiliano wa YAS zamani Tigo wametolewa wasiwasi kuhusiana huduma zilizokuwa zikitolewa na mtandao huo katika ofa na vifurushi kwamba huduma hizo zitabaki kama zilivyokuwa.
Meneja wa YAS zamani Tigo mkoa wa Mara ngudu Rodgers Mbio amesema wanawapongeza wateja wao kwa kukubali na kuwapokea kwa haraka mabadiliko hayo huku akisisitiza mabadiliko hayo ni kwenye chapa tu na hayahusu mambo mengine.
Aidha amesema YAS inaendelea kutoa ofa mbalimbali kuelekea msimu huu wa kufunga mwaka ambapo zipo zawadi ambazo zinatolewa kwa washindi wa kila siku, wiki, mpaka mwezi.
Ikumbukwe kuwa mwezi Nov wamiliki wa mtandao wa mawasiliano wa Tigo Tanzania walibadili chapa ya kutoka Tigo kwenda YAS na kutoka Tigopesa kwenda Mixx by Yas.