Mazingira FM

BUFADESO wahaidi kuwa kinala maonesho ya kilimo mseto Mara

15 November 2024, 12:26 pm

Banda la shirika la Bufadeso kwenye maonesho ya 9 ya kilimo mseto

Baraka amesema kama walivyofanya miaka mingine nyuma na msimu huu wamejipanga kushinda katika maonesho hayo kutokana na ubora wa bidhaa zinazozalishwa na wakulima wao.

Na Adelinus Banenwa

Imeelezwa kuwa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, inaendelea kujenga mazingira wezeshi kwa wakulima kupata elimu na teknolojia bora zitakazochangia kuwa na mifumo endelevu ya chakula na kukuza kipato cha mkulima.

Hayo yamesemwa na Mhe. Dunstan Kitandula  naibu waziri wa maliasili na utalii katika ufunguzi wa maonesho ya tisa ya kilimo mseto mwaka 2024 tarehe 14 novemba 2024 yanayofanyika Bweri Musoma mkoani Mara

Banda la shirika la Bufadeso kwenye maonesho ya 9 ya kilimo mseto

Mhe  Kitandula amesema nchi ya Tanzania inashiriki kwenye mkutano wa makubaliano ya nchi 29 huko Baku, Azerbaijan ili kuweka sauti ya pamoja kwenye kuendeleza uhimilivu wa wakulima wadogo kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, na kilimo mseto ni njia ambayo nchi imeainisha kwenye kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi huku  akiwapongeza wakulima wadogo kwa juhudi zao hizo.

Katika maonesho hayo hayo miongoni mwa mashirika yanayoshiriki ni pamoja na Bufadeso ambapo kupitia kwa Baraka Kamese ambaye ni mratibu washirika hilo amesema wao kama shirika wanayo matumaini makubwa katika maonesho hayo ikiwa ni pamoja na kutoa fursa kwa wakulima wao kupeleka bidhaa mbalimbali walizozizalisha kupitie elimu walioipata.

Banda la shirika la Bufadeso kwenye maonesho ya 9 ya kilimo mseto

Kamese amesema shirika la Bufadeso kama wadau wa kilimo mseto ambapo maonesho ya mwaka huu yana kauli mbiu isemayo Kilimo mseto kwa mifumo endelevu ya chakula na kama Bufadeso wanatembea na kauli hiyo kwa mazao ya wakulima kuyaongezea thamani.

Aidha Baraka amesema kama walivyofanya miaka mingine nyuma na msimu huu wamejipanga kushinda katika maonesho hayo kutokana na ubora wa bidhaa zinazozalishwa na wakulima wao.

Baraka Kamese
Banda la shirika la Bufadeso kwenye maonesho ya 9 ya kilimo mseto

Kwa upande wao wakulima wanaoshiriki katika maonesho hayo walioko chini ya Bufadeso wamesema kwa kiasi kikubwa bidhaa zilizoletwa kwenye maonesho ni zile walizozizalisha kisha kuziongezea thamani kama vile maandazi yaliyotengenezwa kwa unga wa muhogo, wine iliyotokana na asali miongoni mwa bidhaa nyingine

Sauti za wakulima washiriki