Mazingira FM

TAWA yapongezwa mpango wa uvunaji wanyama wakali na waharibifu Bunda

22 October 2024, 1:58 pm

Kiboko aliyevunwa na wahifadhi wa TAWA

Halmashauri ya wilaya ya Bunda kwa siku za hivi karibuni wamekuwa wakipokea matukio mengi ya wananchi kushambuliwa na kuharibiwa mazao yao na wanyama wakali na waharibifu ambao ni mamba na viboko.

Na Adelinus Banenwa

Wakazi wa kata Neruma na maeneo jirani yaliyoko kandokando mwa ziwa Victoria wameishukuru serikali na TAWA kwa mpango wa kuwavuna wanyama wakali na waharibifu hasa mamba na viboko

Wananchi hao wameyasema hayo katika eneo la Namibu ambapo TAWA kwa kushirikiana na wananchi walifanikiwa kumvuna kiboko ambaye wakazi hao wamesema ni miongoni mwa wanyama wasumbufu.

Wakazi wa kata ya Neruma na maeneo jirani wakishuhudia zoezi la TAWA kuendelea na mpango wa kuwavuna wanyamapori wakali na waharibifu

Wakazi hao wameeleza kuwa maeneo ya kandokando mwa ziwa Victoria kutokana na changamoto za wanyama hao wamelazimika kuacha kulima kandokando mwa ziwa baad ya uharibifu wa mazao yao na viboko pia kwa upande wa mamba  zimesababisha kupotea kwa maisha ya watu wengi.

sauti za wananchi
Muhifadhi mwandamizi John Mserekali, ambaye ni kaimu mkuu wa ulinzi wa wanyamapori kanda ya ziwa

Naye muhifadhi mwandamizi John Mserekali, ambaye ni kaimu mkuu wa ulinzi wa wanyamapori kanda ya ziwa amesema mpango huu umekuja baada ya kilio cha wananchi  juu ya uharibifu wa mazao pamoja na kusababisha vifo na majeruhi.

Mserekali amesema wilaya ya bunda inashika nafasi ya tatu kwa matukio ya kilio cha wanyama wakali na waharibifu hasa mamba na viboko hivyo kitondo cha kuanza mpango wa kuwavuna kinalenga kuisaidia jamii kupunguza kilio hicho.

sauti ya JOHN Mserekali
Marwa Kitende mkuu wa Kitengo cha maliasili na uhifadhi wa mazingira kutoka halmashauri ya wilaya ya Bunda

Naye Marwa Kitende mkuu wa Kitengo cha maliasili na uhifadhi wa mazingira kutoka halmashauri ya wilaya ya Bunda amesema kwa siku za hivi karibuni wamekuwa wakipokea matukio mengi ya wananchi kushambuliwa na kuharibiwa mazao yao na wanyama wakali na waharibifu ambao ni Mamba na viboko.

sauti ya Marwa Kitende