TAKUKURU: kumiliki mali zisizoelezeka ni kosa kisheria
22 September 2024, 11:24 am
kwa mujibu wa sheria ya TAKUKURU namba 11 ya mwaka 2007 marejeo mwaka 2022, kugushi nyaraka kwa lengo la kumdanganya muajiri, kumiliki mali zisizoelezeka, matumizi mabaya ya madaraka, kujifanya ofisa wa TAKUKURU ni miongoni mwa makosa yaliyotajwa katika vifungu vya sheria hiyo.
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa kwa wananchi kushiriki katika utoaji wa taarifa za rushwa katika miradi ya serikali inayoendelea.
Hayo yamesemwa na mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Bunda Mussa Ally kwenye kipindi cha ufahamu wa sheria kupia studio za radio Mazingira Fm ambapo amesema kupia miradi inayoendelea wananchi wanayo haki ya kufuatilia na kihoji utekelezaji wake.
Mussa amebainisha kuwa kwa mujibu wa sheria ya TAKUKURU namba 11 ya mwaka 2007 marejeo mwaka 2022 kuna makosa kadhaa yaliyoainishwa ikiwa ni pamoja na matendo ya rushwa katika manunuzi, kugushi nyaraka kwa lengo la kumdanganya muajiri, kumiliki mali zisizoelezeka, matumizi mabaya ya madaraka, kujifanya ofisa wa TAKUKURU miongoni mwa makosa mengine.
Mussa ametamatisha kwa kusema kuwa kuelekea kipindi hiki cha uchaguzi serikali za mitaa jambo lolote linaloashiria vitendo vya rushwa kwa watu wanaotaka kugombea haviruhusiwi na mwananchi yeyote atakayeona vitendo hivyo vinafanyika na hata kwenye miradi asisite kutoa taarifa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU.