Mazingira FM

Ajichoma kisu cha tumbo kwa madai ya kusambazwa mitandaoni

19 September 2024, 2:57 pm

” Kabla ya kumkuta amejichoma kisu asubuhi jana alimeza dawa zangu vidonge saba na akaandika kikaratasi kama wosia akiaga watu yeye anadai eti amesambazwa kwenye mtandao wa tiktok kwamba ni shoga”

Na Adelinus Banenwa

Mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la Magambo Alfred  Festo 50  mkazi wa mtaa wa Saranga kata ya kabarimu  wilaya  Bunda mkoani Mara amenusurika kifo baada ya kujichoma na kisu tumboni ikidaiwa amechoshwa na taarifa za uongo kuhusu yeye zilizosambazwa mtandaoni.

Akizungumza na na radio Mazingira FM Magreth Lucas moja ya wanafamilia wa Magambo amesema tukio hilo la baba yao mkubwa kujichoma kisu limetokea usiku wa kuamkia leo tarehe 19 sep 2024 ambapo watoto wanaoamka kwenda shule ndiyo walio ona damu sebuleni ndipo walipoamshwa na kugundua baba yao mkubwa ndiye amejichoma kisu tumboni.

Magreth ameongeza kuwa kabla tukio la leo baba yao huyo mkubwa yaani Magambo tangu siku ya jana alikuwa akilalamika kuwa watu wanamtuhumu kuwa anajihusisha na mambo ya ushoga na amesambazwa mitandaoni wakati siyo kweli.

Sauti Magreth Lucas moja ya wanafamilia wa Magambo

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa saranga ndugu Philipo Safari ameiambia mazingira fm kuwa ni kweli tukio hilo limetokea ndani ya mtaa wake na taarifa za tukio hilo amezipata alfajiri ya leo na alipofika eneo la tukio na kukuta mwananchi huyo amejichoma kisu aliwasiliana na polisi ambao walimuelekeza ampeleke kwenye matibabu lakini apite kituoni kuchukua fomu namba tau yaani (pf3).

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa wa saranga Philipo Safari

Aidha mwenyekiti safari ametoa wito kwa wananchi kufika ofisi za serikali pindi wanapokuwa na changamoto mbalimbali hata za msongo wa mawazo watawaitia wataalamu kuwasaidia kuliko kuchukua hatua za kujitoa uhai.

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa wa saranga Philipo Safari