Mazingira FM

Mhe Maboto atoa mkono wa pole wahanga wa upepo Sazira

17 September 2024, 2:58 pm

Diwani wa kata ya Sazira na katibu wa mbunge wakipima mahindi ambayo yametolewa na mbunge wa Bunda mjini kuwakabidhi wahanga wa upepo, Picha na Adelinus Banenwa

Wakati mbunge wa jimbo la Bunda mjini akitoa msaada wa mahindi kwa wahanga wa upepo Sazira diwani wa kata hiyo aomba wadau wengine kujitokeza kuwashika mkono

Na Adelinus Banenwa

Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe Robert Chacha Maboto atoa msaada wa mahindi kama mkono wa pole kwa wahanga wa upepo kata ya Sazira halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo kwa niaba ya Mbunge, Emmanuel Kija ambaye ni katibu wa Mhe Maboto amesema Mhe mbunge baada ya kupata taarifa ya madhira hayo ya upepo amechukua hatua ambapo jumla ya gunia 24 za mahindi zimetolewa kwa wahanga hao.

Emmanuel Kija katibu wa mbunge Maboto akizungumza na wakazi wa Sazira mtaa wa Kitaramaka akiwapa pole na kukabidhi msaada uliyotolewa na mbunge, Picha na Adelinus Banenwa

Aidha kija amesema kupitia msaada huo kila kaya iliyoathirika na maafa hayo kwa kata ya sazira inapokea debe moja la mahindi ambapo litawasaidia wananchi wakati serikali ikiendelea na utaratibu wake.

Sauti ya Emmanuel Kija katibu wa mbunge Robert Maboto

Naye diwani wa kata ya Sazira na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Bunda Michael Kweka mbali na kumshukuru mbunge kwa msaada pia amewataka wakazi wa Sazira kuendelea kuwa na ushirikiano hasa kusaidia wale ambao hawana makazi.

Diwani wa kata ya Sazira na katibu wa mbunge wakipima mahindi ambayo yametolewa na mbunge wa Bunda mjini kuwakabidhi wahanga wa upepo, Picha na Adelinus Banenwa
Sauti ya Michael Kweka diwani kata ya Sazira

Kwa upande wao Wakazi wa kata ya sazira halmashauri ya mji wa Bunda wamemshukuru mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe Robert Chacha Maboto kwa kuwapatia msaada wa mahindi wahanga wa upepo katani hapo.

Sauti za wakazi wa kata ya Sazira baada ya kupokea msaada uliotolewa na mbunge wao