Mazingira FM

Mvua ya dakika ishirini yaacha simanzi Sazira nyumba 150 zaezuliwa na upepo

12 September 2024, 4:34 pm

Moja ya nyumba zilizoathirika na mvua iliyokuwa imeambatana na upepo kata ya Sazira, Picha na Adelinus Banenwa

Mvua iliyokuwa imeambatana na upepo yaacha kilio kwa wakazi wa kata ya Sazira halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara baada ya nyumba kama 150 kuezuliwa na upepo na kuacha kaya zaidi ya 135 bila makazi.

Na Adelinus Banenwa

Zaidi ya Nyumba 150 zimeezuliwa na upepo kata ya Sazira halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara kufuatia mvua iliyokuwa imeambatana na upepo mkali iliyonyesha siku ya tarehe 10 Sept 2024 jioni.

Kwa mujibu wa mashuda mvua hiyo iliyonyesha kwa muda mfupi imeacha familia kadhaa bila makazi baada ya nyumba zao kuezuliwa na upepo huo.

Sauti za wahanga wa mvua hiyo

Diwani wa kata ya Sazira na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Bunda Michael Kweka amefanya ziara na kuwatembelea baadhi ya wahanga wa upepo huo na kuwapa pole huku akiomba majirani kuendelea kawapa hifadhi wasio na makazi hadi pale watakapokamilisha marekebisho ya nyumba zao.

Moja ya nyumba zilizoathirika na mvua iliyokuwa imeambatana na upepo kata ya Sazira, Picha na Adelinus Banenwa

Aidha diwani Kweka amesema mbali na athari za nyumba kuezuliwa pia watu wawili walijeruhiwa maeneo mbalimbali ya miili yao kutokana na kudondokewa na matofali ambapo walifikishwa hospitali na kupatiwa matibabu.

Sauti ya Michael Kweka diwani Sazira

Naye mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano akizungumza na wakazi wa mtaa wa Sazira Nyamunyu amesema serikali itafanya tathmini kuona athari zilizopatakani kutokana na mvua iliyonyesha.

Moja ya nyumba zilizoathirika na mvua iliyokuwa imeambatana na upepo kata ya Sazira, Picha na Adelinus Banenwa

Aidha DC Naano amewataka wananchi kuwasaidia wahanga wa tukio hilo ambao makazi yao yameathirika na upepo huo.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Bunda