Baraza la madiwani Bunda DC lalia na RUWASA
8 September 2024, 7:19 pm
Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Bunda wailalamikia wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini RUWASA kwa kusababisha changamoto kubwa ya maji kwenye maeneo ya vijijini.
Na Adelinus Banenwa
Baraza la Madiwani halmashauri ya wilaya ya Bunda limelalamikia Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini RUWASA kwa changamoto ya maji katika maeneo yao.
Diwani wa kata ya Kibara Mhe Mutamwega amesema pamoja na ukubwa wa eneo na idadi ya watu waliopo eneo hilo kumekuwepo na changamoto kubwa ya maji ambapo wananchi wanamaliza hadi mwezi mzima bila huduma ya maji.
Naye diwani wa kata Mugeta amesema mbali na changamoto ya RUWASA kutomaliza miradi yake pia shirika la umeme Tanzania TANESCO kuacha kukata umeme kwa kuwa kimekuwa chanzo cha kuungua kwa pampu za maji katika miradi ya RUWASA.
Amesema mradi wa nyang’aranga umekwama hivyo ametaka kuhakikisha RUWASA wanamaliza mradi huo na wananchi wanapata maji .
Aidha wameziomba mamlaka kama ikiwezekana miradi ya maji iliyoko halmashauri ya wilaya ya Bunda iliyoko chini ya RUWASA ikabidhiwe mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Bunda BUWSSA ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika