Serikali kulipa riba ya asilimia 7 Nyatwali kwa kuchelewesha fidia zao
5 September 2024, 8:28 pm
Zoezi la ulipaji fidia likiwa limefunguliwa rsmi kwa wakazi wa kata ya Nyatwali, mbunge wa Bunda mjini ataka mambo kadhaa yazingatiwe ikiwemo riba ya asilimia saba kutokana na kucheleweshwa kwa fidia zao
Na Adelinus Banenwa
Serikali imeridhia kulipa asilimia saba kama riba ya kuchelewesha ulipaji wa fidia kwa wakazi wa kata ya Nyatwali.
Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Mara Mhe Kanal Evans Mtambi wakati wa zoezi la uzinduzi waulipaji wa fidia kwa wakazi wa Nyatwali leo 5 Sept 2024.
Awali akiwasilisha baadhi ya hoja za wakazi wa Nyatwali Mhe mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe Robert Chacha Maboto amesema pamoja za zoezi la ulipaji wa fidia kuzinduliwa yapo malalamiko ya wananchi ambayo bado hayajafanyiwa kazi.
Mhe Robert Chacha Maboto ameitaka serikali kutoa majibu ya maswali ya wananchi wa kata ya Nyatwari hasa asilimia 7 ambayo ni riba ya kucheleweshwa kwa fidia yao, Eneo la Mjapani, haki ya kuandikishwa kupiga kura miongoni mwa maswali mengine.
Akijibu hoja hizo Kanal Mtambi ameelekeza maeneo yaliyoachwa bila kupimwa likiwemo eneo la magwata, eneo la mjapani na maeneo ya watu wengine yaliyobaki kuhakikisha yote yanapimwa
Sambamba na hilo Mhe Mtambi ameridhia wakazi hao wa Nyatwali kuchukua sehemu ya vifaa vinavyotoka kwenye nyumba ikiwa ni pamoja na mabati, tofali miongoni mwa mali zingine.