Mazingira FM

Vituo 1,597 kutumika uboreshaji daftari la kudumu la INEC Mara

26 August 2024, 9:21 am

Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka tume huru ya taifa ya uchaguzi ndugu Ramadhani Kailima

Vituo 1,597 ni sawa na ongezeko la vituo 50 ukilinganisha na vituo 1,547 vilivyotumika kwenye uboreshaji mwaka 2019/ 2020.

Na Adelinus Banenwa

Jumla ya vituo 1,597 mkoani Mara vimetengwa kutumika kwenye zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka tume huru ya taifa ya Uchaguzi ndugu Ramadhani Kailima katika mkutano wa tume na wadau wa uchaguzi kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura uliofanyika leo 25 Aug 2024.

Kailima amesema idadi hiyo ya vituo 1,597 ni sawa na ongezeko la vituo 50 ukilinganisha na vituo 1,547 vilivyotumika kwenye uboreshaji mwaka 2019/ 2020.

Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Tume huru ya taifa ya uchaguzi

Kailima ameongeza kuwa kwa kuzingatia matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 tume inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 5, 586.433 hii ikiwa ni sawa na asilimia 18.7 ya wapiga kura 29,754,699 waliopo kwenye daftari baada ya uboreshaji uliofanyika mwaka 2019/2020.

Sauti ya Ramadhani Kailima

Aidha amesema vituo 40,126 vitatumika kwenye zoezi la uandikishaji wa daftari la mpiga kura baada ya maboresho 2024, huku vituo 39,709 vikiwa ni Tanzania bara na 417 vikiwa Zanzibar.