Mazingira FM

Watoto kupotea: Wananchi waandamana, mabomu yarindima Lamadi

21 August 2024, 12:40 pm

Wananchi wakiwa wamekaa katikati ya barabara kuu ya Mwanza Musoma eneo la Lamadi wakati wa maandamano mapema leo.

Jeshi la polisi Lamadi wilaya ya Busega mkoani Simiyu limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi wanaoandamana kwenda kituoni hapo na kufunga barabara kuu ya Mwanza – Musoma wakishinikiza kuonana na Mkuu wa Wilaya baada ya watoto kupotea.

Na Edward Lucas

Wakazi wa Lamadi wilaya ya Busega mkoani Simiyu wameandamana hadi katika kituo cha polisi Lamadi wakishinikiza kupata majibu kwa kile kinachodaiwa kutokana na matukio ya watoto kupotea.

Gari la polisi likiimarisha usalama eneo la Lamadi

Mwenzetu Tabia Waziri amefanikiwa kufika katika eneo hilo na kushuhudia kundi kubwa la wananchi wakiwa wametanda katika barabara kuu ya Mwanza Musoma eneo la kituo cha polisi lamadi jambo lililokwamisha wasafiri kuendelea na safari wakishinikiza kuonana na mkuu wa Wilaya kabla ya jeshi la polisi kuwatawanya kwa mabomu ya machozi

Sauti ya tabia waziri akiripoti kutoka eneo la tukio

Mazingira Fm imefanikiwa kuongea na Diwani wa kata ya Lamadi, Bija Laurent Bija ambaye amesema hivi karibuni imeripotiwa matukio mawili ya watoto kupotea ambayo yamechagiza hasira ya wananchi na kuandamana Hadi kituo Cha polisi wakishinikiza kuonana na Mkuu wa Wilaya kwa ajili ya kupata majibu ya  changamoto ya tatizo hilo

Sauti ya Diwani wa kata ya Lamadi, Bija Laurent Bija.

Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Simiyu, inayoongozwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Simon Simalenga, imefika katika eneo hilo na kuimarisha usalama kwa kuwatawanya wananchi hao kwa kupiga mabomu ya machozi.