Mazingira FM

DC Naano aipa kongole Dr. Nchimbi Sec wanafunzi kupata chakula shuleni

15 August 2024, 8:41 pm

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano,Picha na Adelinus Banenwa

Mwanafunzi yeyote ambaye hatachangia chakula shuleni baadhi ya nyaraka zake zitazuiliwa akimaliza kidato cha nne.

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano amewapongeza wazazi na walimu shule ya sekondari Dkt Nchimbi kwa kuwa na muendelezo mzuri wa kuchangia chakula cha wanafunzi shuleni.

Dc Naano ameyasema hayo leo kwenye kikao cha wazazi na walimu kwenye muendelezo wa kupatiana taarifa za mchango wa chakula shuleni na Maendeleo ya taaluma kwa wanafunzi.

Baadhi ya wazazi wa wanafunzi wakimsikiliza mkuu wa wilaya, Picha na Adelinus Banenwa

Dc Naano amesema takwimu zinaonesha shule ambazo zimesimamia suala la chakula shuleni vizuri kwa wanafunzi, shule hizo zimeondoa Ziro na division 4 akitolea mfano shule ya sekondari ya Bunda.

Aidha mhe Naano amesema changamoto kubwa iliyopo kwa matokeo mabaya ya kutaaluma kwenye baadhi ya shule ni kutokuwepo kwa ushilikiano baina ya walimu, wazazi pamoja na wanafunzi hivyo amewaomba wazazi kuendelea kuchangia chakula shuleni na kufuatilia Maendeleo ya watoto huku jukumu  la walimu kufundisha wamuachie yeye atashughulika nalo.

Sauti ya Dc Naano

Awali akiwasilisha taarifa ya mwenendo wa uchangiaji chakula shuleni mkuu wa shule ya sekondari Dkt Nchimbi Mwl. Benard Ngassa amesema shule yake ina jumla ya wanafunzi 1421 huku wanafunzi waliochanga chakula shuleni ni 1016.

Sauti ya Mkuu wa shule Sec Dr Nchimbi

Makamu mkuu wa shule hiyo Mwal. Wilbroad Laurent amesema kupitia kikao cha wazazi cha tarehe 27, May mwaka huu kiliadhimia kuwa suala la chakula shuleni ni agizo halali la serikali hivyo kwa mwanafunzi yeyote ambaye hatachangia chakula shuleni baadhi ya nyaraka zake zitazuiliwa akimaliza kidato cha nne.