Mazingira FM

Waathirika wa tembo walia na malipo yao Bunda

13 July 2024, 7:30 pm

Wananchi Bunda wamekerwa na malipo ya kifuta jasho na kifuta machozi kutokana na madhira ya wanyama waharibifu kuchelewa, wamedai inawachukua hadi miaka mitano, Mbunge Maboto amewatuliza na kusema bunge limeagiza serikali kumaliza tatizo hilo.

Na Adelinus Banenwa

Wananchi wa kata ya Guta katika mitaa ya Tairo na Makongeni wamelalamikia serikali kuchelewa kulipwa kifuta jasho na kifuta machozi kutokana na uharibifu wa wanyama waharibifu wakiwemo tembo na mamba.

Mwananchi akielezea kero ya wananyama waharibifu kwenye mkutano wa mbunge wa Bunda mjini katika kata ya Guta, Picha na Adelinus Banenwa

Malalamiko hayo yametolewa kwenye mkutano wa hadhara wa mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe Robert Chacha Maboto ikiwa nisiku ya tatu ya ziara yake kwenye jimbo la Bunda mjini ambapo kwa siku ya leo July 13, 2024 amefanya ziara kwenye kata ya Guta.

Wananchi hao wamedai kuwa kifuta jasho na kifuta machozi licha ya kuwa ni kidogo lakini pia inachukuwa muda mrefu kulipwa fedha hizo ambapo wananchi hao wamedai wapo baadhi walipata madhira tangu mwaka 2020 lakini hadi sasa hawajalipwa.

Sauti ya wananchi kuhusu kifuta jasho
Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe Robert Chacha Maboto, Picha na Adelinus Banenwa

Akifafanua suala hilo Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe Robert Chacha Maboto amesema suala la kuchelewa kwa kifuta machozi na kifuta jasho ni miongoni mwa maswali aliyoyauliza kwenye vikao vya bunge vilivyomalizika mwezi uliopita kwa kuwa limekuwa changamoto kubwa sana.

Mhe Maboto amesema kupitia ufafanuzi wa serikali ilitaja watu 299 pekee ndiyo waliolipwa na wananchi zaidi  ya 1,100  bado wanadai hali ambayo siyo nzuri.

baadhi ya wananchi wa mtaa watairo kata ya Guta wakimlaki mbunge wao katika ziara ya kutembelea wananchi na kusikiliza kero zao, Picha na Adelinus Banenwa

Amesema kutokana na ukubwa wa jambo hilo bunge lilimuelekeza waziri wa maliasili na utalii kuja na majibu ya namna gani ya kutatua changamoto hiyo kwenye kikao cha bunge cha mwezi wa tisa.

Mhe Mbunge amesema katika suala la wanyamapori waaribifu na   wakali yuko pamoja nao kuhakikisha linapatiwa ufumbuzi na wale wanaodai waweze kulipwa fedha zao.

sauti ya mbunge Mhe Maboto