Mazingira FM

Mitambo: Si kila mwenye cheti cha udereva ni dereva

3 July 2024, 3:09 pm

Kaimu mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Bunda Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Shabani Mitambo, Picha na Adelinus Banenwa

Kuwa na cheti cha udereva kutoka veta au shule ya udereva siyo kigezo cha kuwa dereva

Na adelinus Banenwa

Imeelezwa kuwa si kila mwenye cheti cha kuhitimu mafunzo ya udereva kutoka chuo cha VETA au shule yoyote ya udereva anakuwa amekidhi vigezo vya kuendesha chombo cha moto barabarani, bali ni wale tu waliothibitishwa na ofisi ya mkuu wa usalama barabarani mkoa.

Hayo yamesemwa na kaimu mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Bunda Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Shabani Mitambo alipozungumza na watumiaji wa barabara kupitia Mazingira fm kwenye kipindi cha Asubuhi leo mapema July 3, 2024.

Sauti ya shabani Mitambo
Copl Emmanuel, Picha na Adelinus Banenwa

Kwa upande wake Copl Emmanuel Lagwen kutoka kituo cha polisi Bunda ambaye anahusika na elimu kwa umma amesema vipo visababishi vingi vya ajali ambavyo yamkini vingine vinaweze kuepukika endapo watumiaji wa barabara watazingatia sheria za usalama barabarani.

Copl Emmanuel amesema baadhi ya visababishi vya ajali ni pamoja na, ukungu mkubwa barabarani, mvua kubwa , uterezi katika barabara ambazo niza kiwango cha changarawe, ubovu wa magari miongoni mwa sababu zingine.

Sauti ya Copl Emmanuel Lagwen

Aidha Copl Emmanuel amewataka madereva na watumiaji wote wa vyombo vya moto kuzingatia sheria hasa suala la ubovu wa magari ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.