Mazingira FM

Zaidi ya milion 230 zatolewa kuwakwamua wanawake kiuchumi

21 June 2024, 1:56 pm

Bi Seifu ambae alikuwa mgeni rasmi, akikabidhi fedha za mikopo kwa wanakikundi, Picha na Mariam Mramba

Wanawake watakiwa kujiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali ili viwasaidie kupata mikopo na kujikwamua kimaisha.

Na Mariam Mramba

Jumla ya wanawake 263 kutoka kijiji cha Magunga kata ya Mirwa wilayan Butiama wamenufaika na mkopo wa shilingi (232, 470,000) million mia mbili thelathini na mbili laki nne na sabini elfu kutoka shirika lisilokuwa la kiserikali la mkombozi kwa lengo la kuwawezesha wanawake kiuchumi.

Hayo yamebainishwa kwenye hafla ya uzinduzi wa tawi jipya la shirika hilo la Mkombozi katika kijiji cha Magunga lenye jumla ya vikundi  45 vya wanawake  wanaofanya shuguli zao za ujasiriamali kwa kukopa mikopo modogomidogo kutoka shirika la Mkombozi lenye makao yake makuu  kijiji cha Nyamuswa ndani ya halmashauri ya wilaya Bunda.

Mkurugenzi wa shirika la Mkombozi Hamis Sungura mwenye suti ya bluu, akizungumza kwenye hafla hiyo, Picha na Mariam Mramba

Kwa upande wao wanawake hao wamesema kuwa  kupitia fedha hizo za mikopo wameweza kutoka katika hali duni ya kimaisha,  nakwamba mikopo hiyo wanayoipata inamasharti nafuu nhali inayowafanya  kumudu kurejesha pesa hizokwa urahisi.

Taarifa ya shirika la Mkombozi

Katika hatua nyingine wanufaika  hao wametoa mifuko mitatu ya saruji kwenye ofisi ya kijiji cha Magunga ikiwa ni kuchangia shughuli za maendeleo ya kijiji hicho.

Wanakikundi wa kikundi cha maendeleo Magunga

 Akizungumza katika hafla hiyo Bi Seifu ambae alikuwa mgeni rasmi  ametoa wito kwa wanawake waliopata pesa izo wawe walimu wazuri kwa wanawake wengine huku akitoa viti hamsin, pamoja na fedha taslimu 961,000 ili kutatua changamoto kwa kikundi hicho.

sauti ya Bi Seifu

Kwa upande wa uongozi wa kijiji cha Magunga wamemshukuru mkurugenzi wa shirika la Mkombozi kwa kuwawezesha kina mama hao ambao kupitia fedha hizo za mikopo wamechangia saruji ambayo itasaidia katika shughuli  za ujenzi wa nyumba ya dakitari katika zahanati ya Magunga.

sauti za viongozi wa Magunga