Mazingira FM

Wazazi watakiwa kuzingatia lishe kwa watoto

21 June 2024, 1:19 pm

Albinus Manyama Chikwakala ambaye ni mwenyekiti wa wahudu wa afya ngazi ya jamii, Picha na Catherine Msafiri

Wito umetolewa kwa wazazi na walezi kuzingatia lishe bora kwa watoto chini ya miaka mitano ili kuwa na watoto wenye afya bora

Na Catherine Msafiri

Wazazi na walezi wameaswa kuhakikisha wanazingatia lishe bora kwa watoto wao hasa wa mwaka 0 hadi miaka 5 Ili kuwakinga na utapiamlo na athari zitokanazo na tatizo hilo hayo yameelezwa na Albinus Manyama Chikwakala ambaye ni mwenyekiti wa wahudu wa afya ngazi ya jamii katika maadhimisho ya siku ya lishe ambayo hufanyika kwa mwaka mara mbili.

Akizungumza na Mazingira Fm Chikwakala amesema wao kama watoa huduma za afya ngazi ya jamii huwa wanayoa huduma nyumba Kwa nyumba Ili kuhakikisha wanawahimiza wazazi na walezi katika kuzingatia lishe bora kwa watoto wao na hata familia kwa ujumla.

sauti ya Albinus Manyama Chikwakala

Sambamba na zoezi la utoaji elimu pia kumefanyika zoezi la utoaji matone na dawa za minyoo kwa watoto chini ya miaka 5 Hadi miezi 6 ambapo Veronica Mathias muhudu wa afya ngazi ya jamii anawakumbusha wazazi kujitokeza kupata elimu na watoto wapewe chanjo kwa ni salama na zinawakinga watoto na maradhi mbalimbali.

sauti ya Veronica Mathias

Hata hivyo mwenyekiti wa mtaa wa Saranga Philipo Safari amesema kuwa zoezi hilo la utoaji elimu lishe kwa akina mama linatija na litakuwa endelevu ili kuhakikisha wanawaongoza wananchi wenye afya bora katika jamii.

mzazi akifurahia huku akiwa anawapatia watoto wake uji wa lishe kwenye maadhimisho ya siku ya lishe kata ya Kabarimu.Picha na Catherine Msafiri
sauti ya Philipo Safari
Mhe Muhunda Manyonyoryo, diwani wa kata ya Kabarimu,Picha na Catherine Msafiri

Awali akifungua zoezi hilo mgeni rasmi ambaye ni diwani wa kata ya Kabarimu Mhe Muhunda Manyonyoryo ameeleza mambo matatu ambayo wazazi wanapaswa kuyazingatia katika suala la malezi ya watoto hasa katika kuwapa lishe bora

sauti ya Muhunda Manyonyoryo