Mazingira FM

C-SEMA wapewa hati ya pongezi siku ya wazee

17 June 2024, 2:56 pm

Mwakilishi wa shirika la C-SEMA akipokea hati ya pongezi kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Mara kwenye maadhimisho siku ya kupinga ukatili kwa wazee, Picha na Adelinus Banenwa.

Shirika la C-SEMA lapongezwa utoaji wa elimu ukatili dhidi ya wototo na wenye ulemavu.

Na Adelinus Banenwa

Shirika la C-SEMA limepokea hati ya pongezi katika maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili dhidi ya wazee, yaliyofanyika Juni 15, 2024, wilayani Bunda, mkoani Mara.

Shirika limepongezwa kwa jitihada zake katika kutoa elimu ya kupinga ukatili katika jamii.

Baadhi ya washiriki maadhimisho siku ya kupinga ukatili dhidi ywazee

C-SEMA linajihusisha na programu mbalimbali katika mkoa wa Mara, ikiwa ni pamoja na kupinga ndoa za utotoni na ukeketaji kwa watoto wa kike na watu wenye ulemavu.

Kazi za shirika zinaenea pia katika mikoa mingine yenye changamoto kama vile Manyara, Dodoma, na Kilimanjaro, ambapo ukeketaji una kiwango kikubwa.

Kutoka shirika la C-SEMA kwenye picha ya pamoja baada ya kupokea hati ya pongezi.

Shirika linazingatia juu ya kuhamasisha jamii na kuelimisha kuhusu athari za ukatili na umuhimu wa kupinga mienendo hiyo.

Kupitia mipango yake, C-SEMA inachangia katika kuimarisha haki za binadamu na kuboresha maisha ya watoto na watu wenye ulemavu katika jamii.

Hatua za C-SEMA zinaonyesha jukumu lake muhimu katika kuleta mabadiliko chanya na kukuza uelewa mpana kuhusu haki za binadamu na kutokomeza ukatili.