Mazingira FM

TAKUKURU yawataka wananchi kutambua viashiria vya rushwa kuelekea uchaguzi

11 May 2024, 7:41 pm

Alfred Myalla mkaguzia mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Bunda, Picha na Adelinus Banenwa

TAKUKURU yaanza kujipanga kudhibiti matukio na vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi serikali za mitaa.

Na Adelinus Banenwa

Kujitoa kugombea, kusafirisha wapigakura, kununua au kuuza kadi ya mpiga kura ni miongoni mwa mambo yanayotajwa kuwa ni rushwa  katika kipindi cha uchaguzi.

Hayo yamesemwa na Alfred Myalla mkaguzia mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Bunda katika kipindi cha ufahamu wa sheria kinachorushwa hapa radio Mazingira Fm ambapo amesema TAKUKURU kwa sasa wanatoa elimu kwa wananchi kujua mambo ambayo hayatakiwi katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

Sauti ya Alfred Myalla mkaguzia mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Bunda

Myalla amesema kwa mujibu wa sheria TAKUKURU inayo majukumu makuu matatu ambayo ni, kutoa elimu kwenye jamii kuhusu rushwa, kufanya utafiti kwenye maeneo yaliyokithirika kwa rushwa pamoja na  kufanya uchunguzi wa vitendo vya rushwa.

Alfred Myalla mkaguzia mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Bunda, Picha na Adelinus Banenwa

Aidha Myalla ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za matukio au vitendo vya rushwa kwenye maeneo yao huku akidhibitisha kuwa wao kama TAKUKURU wataendelea kuyafanyia kazi maoni ya wananchi likiwemo la utoaji elimu hasa vijijini.

Sauti ya Alfred Myalla mkaguzia mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Bunda