Mbunge Maboto atoa msaada wa mahindi kwa waathirika wa maji Nyatwali
5 May 2024, 5:41 pm
Ongezeko la kina cha maji ziwa Victoria na wingi wa maji mto Rubana kulivyowaacha mamia ya wakazi wa Nyatwali bila makazi.
Na Adelinus Banenwa
Zaidi ya kaya 360 zimeathirika na maji katika kata ya nyatwali halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara hii ni kwa mujibu wa mkuu wa wilaya ya Bunda Dr. Vicent Naano
Maji hayo ni kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha pamoja na kuongezeka kwa kina cha maji cha ziwa Victoria hali iliyosababisha maji ya ziwa kuingia kwenye makazi ya watu.
Mhe Naano amesema kati ya familia hizo makazi 164 mashamba 156
Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe Robert Chacha Maboto ametoa msaada wa mahindi kwa wakazi wa nyatwali walioathirika na maji katika maeneo yao wapatao 168.
Akizungumza kwa niaba ya mbunge, Emmanuel kija Nkwama Kubuka amesema Mhe mbunge baada ya kupata taarifa za kinachoendelea Nyatwali alifanya juhudi za kuwasiliana na ofisi ya mkuu wa wilaya ambayo kwa pamoja kimepatika chakula kwa nia ya kuwashika mkono wakazi hao.
Aidha katibu wa mbunge amewaomba wadau wengine kujitokeza kuwashika mkono wananyatwali kwa kitu kidogo walichonacho huku akiwataka wakazi hao wa nyatwali kuwa na subra wakati mbunge akiendelea kuwapigania ili wapewe stahiki zao na wawezi kuondoka kwa amani.
Awali wakiwasilisha malalamiko yao mbele ya mkuu wa wilaya wakazi hao wa nyatwali wamemshukuru mhe mbunge kwa msaada aliyowapatia japo ni kidogo lakini kilio chao ni kutaka kujua wanalipwa lini ili waweze kuondoka kutokana na majanga wanayoyapata katika eneo hili na hasa ukizingatia serikali imesimamisha shughuli zote za maendeleo katika kata hiyo
Ikumbukwe kwamba kata ya Nyatwali tayari wakazi wake wamefanyiwa tathmini baada ya serikali kutangaza kulitwaa eneo lote la kata ya Nyatwali kwa maslahi mapana ya nchi na hivyo kulazimika kusimamisha shughuli zote za maendeleo katika eneo hilo.