WWF yabaini vyanzo 578 vya maji Mara
12 March 2024, 12:48 pm
Shirika la WWF katika kutekeleza mpango kazi walioandaa kwa mwaka wa fedha 2024 kwa kuziunga mkono jumuiya za watumia maji mkoa wa Mara, wamebaini vyanzo vya maji zaidi ya 578 ambapo lengo la mradi ni kufikia watu 20,000.
Na catherine Msafiri
Shirika la WWF katika kutekeleza mpango kazi walioandaa kwa mwaka wa fedha 2024 kwa kuziunga mkono jumuiya za watumia maji mkoa wa Mara wamebaini vyanzo vya maji zaidi ya 578 ambapo lengo la mradi ni kufikia watu 20,000.
Hayo yamebainishwa na Enock Edward Mtaigwa afisa Mipango, Tathmini, Mafunzo na Utafiti wa shirikala WWF Tanzania ambapo amebainisha kuwa kwa kutumia vigezo walivyokuwa wanaviangalia kama vile wingi wa maji katika vyanzo, idadi ya watu wanaotumia maji na uwezo wa kuhamisha maji kwenda kwenye vyanzo vingine.
Edward amesema lengo kubwa la mradi huo ni kuhakikisha vyanzo vinatunzwa ili jamii ipate maji safi na ya uhakika kwa matumizi
Aidha Edward amesema katika makundi ambayo walipanga kushirikiana nayo na kuhakikisha wanafanya shughuli mbalimbali katika jamii ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kusaidia jamii upandaji wa miti zaidi ya 16000, kusaidia wakulima kupata mafunzo ya kilimo bora, kubaini vyanzo vya maji na kuweka vigingi na uzio na shughuli zingine kama utoaji wa mizinga ya nyuki kwa jumuiya.
Hata hivyo Edward ameeleza lengo la shirika la WWF Tanzania kwa mwaka huu ilikua ni kupanda miti 7,000 na kuhamasisha miti mingine 9,000 kutoka kwa wadau, lakini mpaka sasa kwa miezi 6 ya mradi tayari wamepanda miti zaidi ya 26,000.
Pia ametoa wito kwa jamii na viongozi wa jumuiya za watumia maji kushiriki kikamilifu katika mradi kwani mradi unapopelekwa katika kijiji unakwenda kuwanufaisha wanakijiji husiki.