Lugha za matusi marufuku kampeni za uchaguzi mdogo Mara
8 March 2024, 4:52 pm
Viongozi wa vyama vya siasa na wafuasi wao wameonywa juu ya matumizi lugha za matusi na kejeli wakati wa kampeni za uchaguzi zinazoendelea katika kata 2 kwa mkoa wa Mara zinazotarajia kufanya uchaguzi mdogo wa udiwani mnamo March 20, 2014 .
Na Adelinus Banenwa

Onyo hilo limetolewa na afisa wa tume ya taifa ya uchaguzi Bi Maria Petro Dadu wakati akifanya mazungumzo na radio Mazingira Fm kuhusu kampeni zinazoendelea kuelekea uchaguzi mdogo wa udiwani.
Bi Maria amesema kwa mkoa wa Mara kata mbili zinashiriki katika uchaguzi huu mdogo wa udiwani, kata hizo ni Busegwe kutoka wilaya ya Butiama na kata ya Mshikamano kutoka wilaya ya Musoma.