Mazingira FM

Mkuu wa uhasibu Serengeti mikononi mwa polisi kwa ubadhirifu

2 March 2024, 5:58 pm

Mkuu wa kitengo Cha uhasibu na fedha halmashauri ya wilaya ya Serengeti yuko mikononi mwa jeshi la polisi mkoani Mara kwa agizo la Mhe waziri Mkuu baada ya kukutwa na tuhuma za kuhamisha fedha za serikali zaidi ya shilingi Milioni 213

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa kitengo Cha uhasibu na fedha halmashauri ya wilaya ya Serengeti yuko mikononi mwa jeshi la polisi mkoani Mara kwa agizo la Mhe waziri Mkuu baada ya kukutwa na tuhuma za kuhamisha fedha za serikali shilingi Milioni 213.748,085 kwa njia ya uhamisho wa ndani na kwenda kuzitumia kwa matumizi binafsi kinyume na makusudio.

Waziri mkuu ametoa agizo kwa Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mara ACP Salum Morcase kumkamata na kuondoka naye ndugu Saad Matunzi Ishabaila kwa tuhuma huzo ambapo yeye binafsi amekili kuhamisha fedha hizo huku ikitatwa kushirikiana na watumishi wengine kitoka TAMISEMI fddha ambazo zilihamishwa kwa awamu nne .

Aidha Mhe Majaliwa amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Samia Suluhu Hasan haitomfumbia mtu yeyote atayebainika kujihusisha na wizi na udokozi kwenye miradi inayoletwa.