NMB yatoa msaada wa vifaa vya shule Rorya vyenye thamani ya milion 84
17 February 2024, 8:59 pm
Mkuu wa wilaya ya Rorya Juma Chikoka ameishukuru Bank ya NMB kuwa wadau wazuri wa maendeleo hasa kwa upande wa elimu.
Na Adelinus Banenwa
Mkuu wa wilaya ya Rorya Juma Chikoka ameishukuru Bank ya NMB kuwa wadau wazuri wa maendeleo hasa kwa upande wa elimu.
Dc Chikoka ameyasema hayo leo wakati akipokea msaada wa vifaa mbalimbali vya sekta ya elimu kwa shule tano tofauti vyenye thamani ya shilingi milioni 84.
Kwa upande wake kaimu Meneja wa NMB kanda ya ziwa Hamadani Silia amesema wao kama banki na wadau wa maendeleo hasa katika sekta ya elimu baada ya kupokea maombi wamechangia vifaa hivyo ili kurudisha faida kwa wananchi ambao pia ndiyo wateja wao.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na madawati, mabati, pamoja na vifaa vingine vya ujenzi kwa shule tano tofauti wilayani Rorya ambavyo thamani yake ni shilingi milioni 84.
Diwani kata ya Nyahongo Samson Kagutu amesema NMB wamekuwa wadau wazuri wa maendeleo ambapo amesema katika shule mbili atajitolea kuwafungulia akaunti wanafunzi 10 kutoka katika kata ya Nyahongo ili ushirikiano uonekane.