Watumishi wa mahakama Bunda watoa msaada wa magodoro gereza la Bunda
1 February 2024, 4:15 pm
Mahakama ya wilaya ya Bunda kwa kushirkiana na wadau wa masuala ya sheria wametoa msaada wa magodoro kwenye gereza la Bunda.
Na Adelinus Banenwa
Mahakama ya wilaya ya Bunda kwa kushirkiana na wadau wa masuala ya sheria wametoa msaada wa magodoro kwenye gereza la Bunda.
Akizungumza katika kukabidhi msaada huo Mhe hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Bunda Mulokozi Paschal Kamuntu amesema wao kama wadau wa sheria kwenye wiki hii ya sheria wamewiwa kutoa msaada huo ili kuonesha mchango wao .
Mhe Kamuntu amesema kilele cha wiki ya sheria kwa wilaya ya Bunda itafanyika siku ya tarehe moja mwezi Feb 2024 katika viwanja vya mahakama ya wilaya huku akibainisha kuwa katika kipindi cha wiki nzima elimu mbalimbali za masuala ya kisheria zimetolewa.
Kwa upande wake Mkuu wa Gereza la Bunda Fredrick Mpokwa ameishukuru mahakama kwa msaada walioutoa kwa kuwa utawasaidia pakubwa huku akitoa rai kwa wadau wengine kuguswa na kundi hilo.