Bunda wapewa tahadhari ugonjwa wa Kipindupindu
11 January 2024, 1:10 pm
Katibu tawala wilaya ya Bunda Salumu Mtelela amewata wananchi wilayani Bunda kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa kipindupindu baada ya kuripotiwa mikoa jirani.
Na Adelinus Banenwa
Katibu tawala wilaya ya Bunda Salumu Mtelela amewata wananchi wilayani Bunda kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa kipindupindu baada ya kuripotiwa mikoa jirani.
Wito huo ameutoa maeneo ya stendi ya zamani mjini Bunda akiambatana na kamati ya ulinzi na usalama Kwa lengo la kuhamasisha wananchi kuzangatia usafi wa Mazingira.
Ndugu Mtelela amesema wananchi wahakikishe wananawa mikono kabla ya kula chakula chochote hata kama ni matunda ili kujiepusha na ugonjwa wa kipindupindu.
Kwa upande wake afisa afya kutoka halmashauri ya mji wa Bunda Ndugu Wilfred Morrison Gunje amesema kutokana na maelekezo ya mkuu wa wilaya ya Bunda wameanzisha ukaguzi wa maeneo yote ya biashara na makazi ya watu kuhakikisha watu wote wanazingatia usafi
Aidha amesema katika ukaguzi huo pia wanaangalia suala la vyoo bora na matumizi ya vifaa maalumu vya kutuunzia taka (Dustbeen) katika maeneo yao huku akibainisha kwa wale wote wenye kukiuka utunzaji wa mazingira sheria inataja faini ya elfu hamsina hadi laki tatu.