Mazingira FM

Wahudumu wa afya Bwai walia na hatari ya magonjwa wananchi kukosa huduma ya vyoo

22 November 2023, 5:05 pm

Vichaka na kandokando ya ziwa vimeendelea kutumika kama vyoo jambo ambalo ni hatari kwa afya hasa kwa kipindi hiki cha mvua.

Na Edward Lucas

Wahudumu wa afya kijiji cha Bwai Musoma Vijijini walia na hatari ya magonjwa ya tumbo na magonjwa mengine ya mlipuko kutokana na wananchi kukosa huduma za vyoo katika makazi yao.

Wakizungumza na Radio Mazingira Fm kwa nyakati tofauti wamesema licha ya juhudi zinazofanywa bado wananchi wamekuwa na magonjwa ya kujirudia rudia ambayo baadhi yanasababishwa na wananchi kukosa huduma za vyoo bora na kujisaidia hovyo katika mazingira.

Wamesema hali hiyo imekuwa ikiwafanya watu wengi kufika zahanati kutokana na magonjwa ya tumbo na hata baada ya matibabu bado hawazingatii kanuni za afya na maelekezo ya wataalamu.

Sauti ya wahudumu wa afya katika kijiji cha Bwai

Naye Mhudumu wa Afya ngazi ya Jamii CHW kijiji cha Bwai, Stephano Kang’oma akizungumzia changamoto hiyo amesema hatari kubwa iko kwa wananchi wanaofanya shughuli zao mwaloni na kuomba ofisi ya Mkurugenzi iwawezeshe kupata huduma ya choo ili kuepuka milipuko ya magonjwa.

Stephano Kang’oma, mhudumu wa afya ngazi ya jamii (CHW) kijiji cha Bwai
Sauti ya Stephano Kang’oma

Aidha katika hatua nyingine, Mazingira Fm imezungumza na Mwenyekiti wa kijiji cha Bwai-Kumsoma, Pima Masinde ili kubaini hatua zinazochukuliwa ambapo amesema wamewasilisha ombi halmashauri iwaongezee fedha kwa ajili ya ujenzi wa choo kwani kiasi cha shilingi milioni 5 waliopewa bado hakitoshi.

Pima Masinde, Mwenyekiti wa kijiji cha Bwai-Kumsoma Wilaya ya Musoma Vijijini
Sauti ya Pima Masinde, Mwenyekiti wa kijiji