DC Naano aitaka halmashauri Bunda Mji kutatua migogoro ya ardhi na kulipa fidia
12 November 2023, 11:47 am
Dkt. Anney ameielekeza Halmashauri kufanyia kazi migogoro yote ya ardhi hasa iliyopo katika maeneo ya Taasisi kwa kulipa fidia wananchi waliohamishwa katika maeneo hayo.
na adelinus Banenwa
Dkt. Anney ameielekeza Halmashauri kufanyia kazi migogoro yote ya ardhi hasa iliyopo katika maeneo ya Taasisi kwa kulipa fidia wananchi waliohamishwa katika maeneo hayo akitolea mfano wa Eneo la EPZ, Shule ya Msingi Nyerere na Manyamanya.
Maelekezo hayo ameyatoa katika mkutano wa baraza la madiwani wa roba ya kwanza halmashauri ya mji wa Bunda uliofanyika Nov 9, 2023.
Aidha, DC Naano ameielekeza Halmashauri kushughulia madeni ya Wastaafu wote wanaodai pamoja na madeni ya wananchi walioshinda kesi mahakamani dhidi ya Halmashauri hiyo.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amesisitiza kuongeza umakini katika suala la ukusanyaji mapato huku akibainisha upotevu mkubwa hasa katika maeneo ya minada. Pia amekemea suala la wizi na kuitaka Menejimenti kuwafuatilia kwa umakini watumishi ambao siyo waadilifu katika ofisi zao hasa katika upande wa manunuzi manunuzi.
Katika hatua nyingine mhe mkuu wa wilaya ameonya suala la wizi na udokozi mitaani huku akipiga marufuku kuzurula usiku kuanzi saa tano na endapo mtu atabainika katika muda huo bila sababu ya msingi hatua zitachukuliwa dhidi yake
Dc Naano amesema hatua hiyo inalenga kuweka usalama wa raia na mali zao katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka
Katika kikao hicho pia baraza la madiwani lilipokea taarifa za utekelezaji wa miradi mbalimbali inayosimamiwa na mamlaka za serikali ikiwepo TARURA, BUWSSA, TANESCO pamoja na TASAF.