Wilaya ya Bunda kulima ekari elfu 69 za pamba msimu huu
1 November 2023, 9:15 am
Kiasi cha ekari elfu 69,110 za zao la pamba zinatarajiwa kulimwa ndani ya wilaya ya Bunda katika katika msimu wa mwaka 2023 – 2024.
Na Adelinus Banenwa
Kiasi cha ekari elfu 69,110 za zao la pamba zinatarajiwa kulimwa ndani ya wilaya ya Bunda katika katika msimu wa mwaka 2023 – 2024.
Hayo yamesemwa na mkaguzi wa zao la pamba wilaya ya Bunda kutoka bodi ya pamba Tanzania ndugu Hemed Kabea wakati anazungumza na mazingira fm huku akibainisha kuwa hadi sasa wamepokea mbegu za pamba kilo laki sita ambazo zinatosha kupanda ekari elfu 65.
Aidha kabea amesema kwa sasa wakulima wamebadirika kutokana na mabadiriko ya tabia ya nchi ambapo awali walikuwa wakipanda zao la pamba kwa mujibu wa kalenda ya bodi ni kuanzia tarehe 15 nov hadi tarehe 15 dec lakini kwa sasa wakulima wanapanda kuanzia mwezi wa wa 9 tarehe 10.