Mazingira FM

Wakazi 5000 kunufaika na mradi wa maji Manyamanyama, Mugaja

1 November 2023, 9:24 am

Mkurugenzi wa BUWSSA, Bi Esther Giryoma katika mradi wa maji Manyamanyama Mugaja, Picha na Adelinus Banenwa

Zaidi ya wakazi 5000 kutoka kata ya Manyamanyama na maeneo jirani wanatarajia kunufaika na huduma ya maji kutoka mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Bunda BUWSSA.

Na Adelinus Banenwa

Zaidi ya wakazi 5000 kutoka kata ya Manyamanyama na maeneo jirani wanatarajia kunufaika na huduma ya maji kutoka mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Bunda BUWSSA baada ya kukamilika kwa mradi unaotekelezwa unaotambulika kama Manyamanyama Mgaja.

Hayo yamesemwa na mkurugenzia mtendaji wa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Bunda BUWSSA Bi ESTHER GIRYOMA ambapo amesema mradi huu unathamni ya shilingi bilioni 1.1 na tenki linalojengwa litakuwa na ujazo wa lita laki moja (100,000 LT).

baadhi ya shughuli zinazoendelea katika mradi, Picha na Adelinus Banenwa

Aidha Bi GIRYOMA amesema kutokana na mahitaji ya maji katika eneo hilo BUWSSA wanatarajia ifikapo tarehe 10 mwezi wa 12 mwaka huu wakazi wa Manyamanyama na viunga vyake wawe wameshapata maji hayo.

Mkurugenzi wa BUWSSA, Bi Esther Giryoma

Naye muhandisi Jumanne Seleli mkurugenzi wa usambazaji maji kutoka BUWSSA amesema mradi huo umeanza kutekelezwa mwezi wa tisa ambapo kazi ya kuchimba mitaro yenye urefu wa kilometa saba na ulazaji mabomba tayari umekamilika.

Eneo linapojengwa tenki

Aidha Eng Jumanne amesema dhumuni la Buwssa ni ifikapo 2025 wakazi wa Bunda asilimia 95 wawe na maji safi na salama ambapoa amesema hadi sasa wamefikia asilimia 78.

Jumanne Seleli mkurugenzi wa usambazaji maji kutoka BUWSSA

Kwa upande wao wakazi wa manyamanyama wamesema changamoto ya maji katika eneo lao ni kubwa sana ambapo hulazimika kuamka usiku kutafuta maji ama kwenye visima na madibwi huku wakikumbana na adha mbalimbali ikiwemo kushambuliwa na wanyama kama vile fisi na mbwa.

Wananchi wakishiriki katika mradi, Picha na Adelinus Banenwa
MWANANCHI