Mazingira FM

Wakazi Migungani walalamikia uzururishaji mifugo kwenye maeneo yao

22 September 2023, 4:01 pm

Mhe Diwani wa kata ya Bunda stoo Flavian Chacha, Picha na Adelinus Banenwa

Wakazi wa mtaa wa Migungani kata ya Bunda stoo wameitaka serikali ya mtaa kuwasimamia wafugaji ili waache kuzururisha mifugo katika maeneo yao.

Na Adelinus Banenwa

Tatizo la mufugo kuzurura mitaani, upungufu wa huduma ya maji, na wananchi kutohudhuria vikao ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili wakazi wa mtaa wa Migungani kata ya Bunda Stoo halmashauri ya Mji wa Bunda

Changamoto hizo zimeibuliwa katika ziara ya Mhe Diwani wa kata ya Bunda stoo Flavian Chacha anayoendelea nayo katika kata yake kutembelea mitaa na kusikiliza kero za wananchi.

Katika mkutano huo wananchi wa mtaa wa Migungani wamesema changamoto ya mifugo kuzurura mitaani na kuchunga kwenye maeneo yao limekiwa tatizo kubwa huku wakiwatupia lawama wachungaji wa mifugo hiyo kuwa na viburi

Akitolea ufafanuzi wa changamoto hizo Mhe Diwani amesema Kwa mujibu wa sheria za halmashauri ya mji wa Bunda haitakiwi mtu kuchunga mifugo katika maeneo yaliyoko mjini na adhabu zake zipo ikiwa ni kutozwa faini zipo Kwa mujibu wa sheria

Katika hatua nyingine Mhe Flavian amefafanua juu ya utekelezaji wa miradi mingine ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara za mitaa, huduma ya maji, changamoto ya tembo miongoni wa mambo mengine.