Wananchi Butakale walia na huduma za maji, barabara
29 August 2023, 10:41 am
Wakazi wa mtaa wa Butakale kata ya Bunda Stoo halmashauri ya mji wa Bunda wamelalamikia changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama pamoja na changamoto ya tembo katika maeneo yao.
Na Adelinus Banenwa
Wakazi wa mtaa wa Butakale kata ya Bunda stoo halmashauri ya mji wa Bunda wamelalamikia changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama pamoja na changamoto ya tembo katika maeneo yao.
Wakizungumza katika kikao cha Mhe diwani wa kata hiyo Flaviani Chacha Nyamegeko aliyefika katika eneo la Malangaleni kusikiliza kero za wananchi na kuelezea mipango ya maendeleo katika eneo hilo wananchi wamesema kikwazo kikubwa kwao kwa sasa ni suala la barabara, maji na changamoto ya tembo.
Kwa upande wake Mhe Flaviani Chacha amewatoa hofu wananchi kuhusu suala la maji kwa kuwa Rambo walilolichimba wananchi yeye kama diwani kwa kushirikiana na mbunge wa jimbo la bunda mjini Mhe Robert Mabotto watahakikisha wanaleta mtambo (greda) kwa ajili ya kupanua Rambo hilo ili maji yanayovunwa yawe na uwezo wa kukaa mwaka mzima huku wakingojea mpango wa kusambaza maji kupitia mamlaka ya maji Bunda BUWASSA
Katika hatua nyingine Mhe Flaviani amesema suala wanyama tembo limekuwa sugu hasa kulipa kifuta jasho na kifuta machozi kwa waathirika wa wanyama hao licha ya kuwa amelipigia kelele sana lakini changamoto bado ni kubwa hasa ucheleweshwaji wa fedha hizo pia fedha zenyewe kuwa kidogo.