Mazingira FM

Bunda kinara wizi wa fedha za miradi ya maendeleo mkoani Mara

25 April 2023, 4:24 pm

RC MARA SULEIMA MZEE

Imeelezwa kua katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali mkoani Mara  Wilaya ya Bunda inaongoza kwa wizi wa vifaa vya ujenzi  wa miradi  hiyo jambo ambalo linarudisha nyuma juhudi za serikali.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa Mkoa wa Mara  Meja jenerali Sulemani Mzee katika ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa chujio la maji  Nyabehu  wenye gharama ya zaidi ya Tsh.  bilioni 10 na ambao utanufaisha wakazi wote wa wilaya Bunda pindi utakapo kamilika.

Akiwa katika eneo la mradi huo RC Mzee amesema suala la wizi katika miradi ya serikali linasikitisha hasa wilaya ya Bunda na kuwataka wananchi kuwa walinzi wa miradi hiyo.

SULEIMAN MZEE RC MARA

Hata hivyo mkuu wa mkoa amewapongeza  BUWSSA kwa kazi nzuri ambayo wanaendelea kuifanya katika kutekeleza mradi huo huku akiwata wasimamizi kurekebisha sehemu zenye kasoro ili kuendana na thamani ya pesa inayotolewa naserikali.

SULEIMAN MZEE RC MARA

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Bunda Dr. Vicent Naano amemshukuru mh. Rais Samia Suluhu Hassan  kwa kuwezesha ujenzi wa chujio hilo huku akiwataka BUWSSA kuweka mfumo wa kisasa wa ulinzi utakao saidia kudhibiti uharibifu wa mradi huo.

DR. VICENT NAANO DC BUNDA

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji  safi na usafi wa mazingira Bunda BUWSSA Ester Gilyoma amesema utekelzaji wa mradi huo umefikia asilimia 99 na sasa wananchi wanapata maji safi na salama tofauti na ilivyo kua awali.