Mashindano ya Taifa ya mpira wa mikono yafanyika Bunda Mji
10 April 2023, 8:11 am
Kwa mara ya pili mfululizo mashindano ya mpira wa mikono (handball) Taifa yanafanyika katika ardhi ya Halmashauri ya Mji wa Bunda.
Mashindano haya yalianza siku ya Jumatano tarehe 04.04.2023 na kuzinduliwa na mdau mkubwa wa michezo Ndg. Kambarage Wasira katika viwanja vya shule ya Msingi Miembeni.
Viongozi mbalimbali wamehudhuria kushuhudia mtanange huu wakiongozi na mwenyeji wao Afisa michezo wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Mwl. Amossy Mtani pamoja n.a. Katibu wa Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Peluth Kiranga.
Ikumbukwe kwamba mshindi wa mashindano haya atakwenda kuiwakilisha nchi yetu katika mashindano ya Afrika mashariki na Kati yatakayofanyika katika nchi yetu.
Timu zilizoshiriki ni Ngome JWTZ (Me na Ke), JKT (Me na Ke), Timu kutoka Mwanza na timu kutoka Mara kama wenyeji.
Mashindano hayo yamekamilika siku ya Jumamosi tarehe 08.04.2023 ambapo timu ya Jeshi la wananchi makao makuu (Ngome) imeibuka mshindi ikiwa inatetea taji lake baada ya mwaka Jana kuibuka mshindi katika fainali hiyo.