Mazingira FM

Malibwa, Wazazi na walezi watakaoshindwa kupeleka watoto wao shule kukamatwa

9 January 2023, 9:43 pm

Wazazi na walezi kata ya Nyamakokoto katika Halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara wametakiwa kuwapeleka watoto wao shule na ambao hawatafanya hivyo watakamatwa.

 

Hayo yamebainishwa leo na Diwani wa kata ya Nyamakokoto Mhe, Emmanuel Malibwa wakati akizungumza na Radio Mazingira Fm alipofika shule ya sekondari ya nyamakokoto kuona namna uandikishaji wanafunzi kidato cha kwanza unavyokwenda.

”Tutamkamata mzazi yeyote atayeshindwa kumpeleka mtoto wake shule bila sababu narudia tena tutawakamata haiwezekani serikali itengeneze miundombinu ya shule  madawati yapo madarasa yapo afu mzazi kwa makusudi ashindwe kuleta mtoto shule kama unatatizo lolote njoo na mtoto muone mwalimu hapa shuleni atakusikiliza”  Amesema Malibwa.

”Ndugu muandishi wa habari natoka shule ya sekondari ya Nyamakokoto nakwenda kuzungukia shule zangu zote za msingi kubaini changamoto zilizopo ila naendelea kutoa wito kwa wazazi pelekeni watoto shule mpe mtoto urithi wa elimu leo unanihoji mimi kwa sababu wazazi wangu walinipeleka shule”

Ikumbukwe shule ya sekondary ya nyamakokoto ni miomgoni mwa shule tatu wilayani Bunda ilipokea fedha kutoka serikalini shilingi milioni 470 katika ujenzi wake awamu ya kwanza ambapo awamu ya pili itapokea shilingi milioni 130 ili kukamilika.